Advertisements

Thursday, March 28, 2024

MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILKI ZA ARDHI NZEGA MJINI KUKAMILIKA JUNI 30, 2024


Na Eleuteri Mangi
Utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP)katika Halmashauri ya Mji Nzega katika mkoa wa Tabora umetekelezwa kwa asilimia 55 na kutarajiwa kukamilika Juni 30, 2024.

Akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Japhet Hasunga na ujumbe wake wakati wa ziara ya Kamati hiyo wilayani Nzega tarehe 27 Machi 2024, Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Geophrey Pinda amesema utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi katika mji wa Nzega unatekelezwa katika mitaa 14 iliyopo Kata za Nzega Mashariki, Nzega Magharibi, Nzega ndogo, Kitangiri na Uchama.

Amebainisha kuwa, katika kata ya Nzega Mjini Mashariki mradi unatekelezwa Mitaa ya Maporomoko, Uwanja wa Ndege, Msoma, Mwaisela, Nyasa pamoja na Kitongo. Aidha, Kata ya Nzega Mjini Magharibi mradi unatekelezwa katika mitaa ya Ipilili, Mbugani, Ushirika na Utemini.

Aidha, kwa upande wa Kata ya Nzega ndogo mradi unatekelezwa kwenye mtaa wa Zogolo. Kata ya uchama mradi unatekelezwa katika Mtaa wa Uchama na kwa kata ya Kitangiri Mradi unatekelezwa Mitaa ya Kitangiri na Budushi.

Awali akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kuhusu utekelezaji wa mradi huo, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema katika halmashauri ya Mji wa Nzega mradi ulianza kutekelezwa Novemba, 2023 kwa lengo la kurasimisha vipande vya ardhi 20,000 na kuongeza Alama za Msingi za Upimaji 14.

KUSUASUA UJENZI LAINI YA UMEME TABORA-URAMBO KWAMSIKITISHA DKT. BITEKO


-Aagiza Meneja Mkuu ETDCO kuondolewa
- Azitaka Taasisi za Wizara ya Nishati wasifanye kazi kwa mazoea
-Asema Watendaji wasioweza kuishi Maono ya Rais Samia wajitafakari

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amekagua mradi wa ujenzi wa Kituo cha Kupoza umeme cha Uhuru kilichopo wilayani Urambo mkoani Tabora na kueleza kutoridhishwa kwake na kazi ya ujenzi wa laini ya msongo wa kV 132 kutoka Tabora hadi Urambo ambayo inatekelezwa na kampuni tanzu ya TANESCO (ETDCO).

Kazi ya ujenzi wa Kituo cha kupoza umeme cha Uhuru imegawanyika katika sehemu mbili ambapo ujenzi wa kituo cha kupoza umeme unafanywa na kampuni ya TBEA kutoka China ambao wamefikia asilimia 84 ya utekelezaji huku kazi ya ujenzi wa laini ya umeme kutoka Tabora hadi Urambo (km 115) ikifanywa na kampuni ya ETDCO ambao wamefikia asilimia 10 tu ya utekelezaji.
Kufuatia hali ya kusuasua kwa ujenzi wa laini hiyo, Dkt. Biteko ameiagiza Bodi ya TANESCO kumwondoa Meneja Mkuu wa ETDCO Muhamed Abdallah ambaye ameonekana kutotoa kipaumbele katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayosimamiwa na Kampuni hiyo.

“Tarehe 17 Septemba, 2023 nilimtuma Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga kuja kukagua mradi huu ambaye aliwapa maelekezo ya kukamilisha mradi, pia nilimtuma aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO, Meja Jenerali Paul Simuli kuja kukagua mradi huu 17 Desemba 2023 naye alitoa maelekezo ambayo hayajatekelezwa, hatari iliyopo hapa ni kuwa TBEA atakamilisha kazi mapema mwezi Juni lakini umeme bado hautapatikana kwenye kituo kwa sababu laini ya umeme itakuwa haijakamilika.” Amesema Dkt. Biteko

DHAMIRA YA SERIKALI NI KUKUZA UCHUMI WA SEKTA BINAFSI KWA KUWEKA MAZINGIRA WEZESHI: BASHUNGWA


Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ameeleza kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ni kukuza uchumi wa Sekta binafsi inayochangia makusanyo ya kodi ambazo zitawezesha ujenzi wa miundombinu ya barabara na utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo nchini.

Bashungwa amezungumza hayo Machi 27, 2024 katika kikao kilichowakutanisha wafanyabiashara wa Wilaya ya Karagwe pamoja na Taasisi za Serikali zinazowahudumia ambapo amesikiliza kero zao ikiwemo tozo kubwa za kodi, ushuru pamoja na kauli zisizoridhisha kutoka kwa Maafisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA).
Bashungwa amesisitiza kuwa ukusanyaji wa mapato unawezesha Serikali kufanikisha malengo yake ya kuhudumia nchi pamoja na wananchi wake kwa haraka kwa kuwa wajibu wa Serikali ni kujenga ustawi wa wafanyabiashara na sio kuwadumaza.

“Sijafurahishwa na madai ya kauli za Maafisa kwa wafanyabiashara ambazo sio sahihi,kwa kuwaaambia wakishindwa kulipa kodi, wafunge baishara, Lengo la Serikali ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwawezesha kwa kutoa elimu, kuwashauri na kustawisha wafanyabiashara” amesisitiza Bashungwa.

Wednesday, March 27, 2024

RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AFUTURISHA VIONGOZI PAMOJA NA MAKUNDI MBALIMBALI IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa Futari mtoto Yatima Shuraiya Ramadhan (6) wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma. Rais Samia aliwaandalia Iftari Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpakulia Iftar mtoto Yatima Shuraiya Ramadhan (6) wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma. Rais Samia aliwaandalia Iftar Viongozi pamoja na Wageni mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Iftar aliyowaandalia Viongozi pamoja na Makundi mbalimbali Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaji Mustafa Rajab Shaban kwenye picha na Watoto Yatima Shuraiya Ramadhan, Dhul-kaya Ramadhan pamoja na Ikramu Selemani wa Kituo cha Watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Jijjini Dodoma mara baada ya kufuturu Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amebeba Kombe la Ubingwa wakati wa picha ya pamoja na Vijana wa Ramadhan Brothers ambao waliibuka washindi wa shindano la America’s Got Talent (AGT) mara baada ya Iftar Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 27 Machi, 2024.

TCAA YAFUTURISHA NA KUTOA MKONO WA EID KITUO CHA BUSARA



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akipata futari Pamoja na Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.

Sheikh Issa Othman akitoa neno wakati wa futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akiongoza menejimenti ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga kukabidhi mkono wa Siku Kuu ya Eid kwa Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Hamza Johari akifuturu na  Watoto wanaolelewa katika kituo cha Busara kilichopo Banana jijini Dar es Salaam wakati wa futari iliyoandaliwa na TCAA.

WAZIRI DKT. NCHEMBA AKUTANA NA MKURUGENZI MPYA WA TBL


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipeana mkono na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, baada ya kufika Ofisi za Hazina (Treasury Square), jijini Dodoma, kujitambulisha, ambapo Mkurugenzi Mtendaji huyo ameipongeza Serikali kwa kuboresha mazingira ya kufanyabiashara na kuahidi kuwa Kampuni yake itaendelea kuchangia maendeleo ya nchi kupitia program mbalimbali za kusaidia jamii na kulipa kodi.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), kushoto, akisikiliza maelezo ya Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (kulia), kuhusu Kampuni yake kuendelea kuchangia maendeleo ya jamii, alipofika kujitambulisha, katika ukumbi wa Mikutano wa Waziri (Treasury Square), jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akizungumza jambo wakati wa mkutano wake na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hayupo pichani), baada ya kufika kujitambulisha, ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma, ambapo amepongeza jitihada za Serikali za kuimarisha Sera zinazoweka mazingira bora ya ufanyaji biashara.
Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin, akizungumza kuhusu mchango wa Kampuni yake katika maendeleo ya uchumi, alipofika kujitambulisha kwa Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma.
Kamishna wa Idara ya Sera, Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, akifafanua jambo kuhusu Sera ya fedha wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) na Mkurugenzi Mtendaji mpya wa Kampuni ya Tanzania Breweries Pls, Bi. Michelle Kilpin (hawapo pichani), kushoto kwake ni wajumbe wa mkutano huo kutoka Wizara ya Fedha, jijini Dodoma.

WAZIRI JAFO AZUNGUMZIA MAFANIKIO YA MIAKA 60 YA MUUNGANO


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Dodoma
Waandishi wa habari wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Dodoma leo Machi 26, 2024, Dodoma.
Waandishi wa habari wakifuatilia kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo (hayupo pichani) kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi (kulia) na Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Mobhare Matinyi wakati wa kikao na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka 60 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jijini Dodoma leo Machi 26, 2024, Dodoma. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Bi. Sarah Kibonde.

DKT. BITEKO AZINDUA KIWANDA CHA KUWEKA MIFUMO YA UPASHAJI NA UTUNZAJI JOTO MABOMBA YA EACOP


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (katikati) akisalimiana na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Ruth Nankabirwa kabla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha na kutunza joto katika mabomba yatakayosafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga kupitia Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Kiwanda kipo Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akiwa katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha na kutunza joto katika mabomba yatakayotumika kusafirisha mafuta ghafi
kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga kupitia Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Kiwanda kipo Sojo wilayani Nzega mkoani Tabora.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kuweka mifumo ya kupasha na kutunza joto katika mabomba yatakayosafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga kupitia Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Kushoto kwake ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhe. Ruth Nankabirwa na kkulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato.

KIJANA ABELI AMKOSHA DKT. NCHEMBA KWA SANAA YA UCHORAJI


Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akipokea picha kutoka kwa Msanii wa Uchoraji kutoka jijini Dar es Salaam, Bw. Abel Mndeba, aliyefika kijana huyo mkazi wa mkoani Mbeya anayefanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amechukua uamuzi wa kuchora picha kwa kutambua mchango mkubwa wa Mhe. Dkt. Nchemba katika kukuza maendeleo ya nchi katika sekta za huduma za jamii na kiuchumi kupitia utafutaji wa rasilimali fedha zunazotumiwa na Sekta za utekelezaji wa miradi mbalimbali inayoendelea hapa nchini.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akiwa katika picha na Msanii wa Uchoraji, Bw. Abel Mndeba, aliyefika ofisini kwake kukabidhi zawadi ya picha yake ya kuchora, ambapo kijana huyo mkazi wa mkoani Mbeya anayefanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam, amesema kuwa amechukua uamuzi huo kwa kutambua mchango mkubwa wa Mhe. Dkt. Nchemba katika kukuza maendeleo ya nchi katika sekta za huduma za jamii na kiuchumi kupitia utafutaji wa rasilimali fedha zinazotumiwa na Wizara, Idara na Taasisi za Serikali kwenye miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), akisikiliza maelezo ya Msanii wa Uchoraji kutoka jijini Dar es Salaam, Bw. Abel Mndeba, aliyefika ofisini kwake (Treasury Square), jijini Dodoma kukabidhi zawadi ya picha ya Mheshimiwa Waziri inayoelezea utendaji kazi wake mahili katika kusimamia masuala ya uchumi, fedha, ustawi wa jamii na nchi kwa ujumla.

POLISI YAJIPANGA KUIMARISHA ULINZI SIKUKUU YA PASAKA



WANANCHI WASISITIZWA KUTUMIA KWA USAHIHI MIUNDOMBINU YA MAJITAKA


MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kushoto) akiwa na Diwani wa Kata ya Majengo, Shufaa Ibrahim (haonekani) wakikagua miundombinu ya majitaka katika eneo hilo Machi 26, 2024 wakati wa kutembelea kata hiyo na kujionea hali ya mazingira ilivyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Bernard Rugayi. (Picha na Mpigapicha Wetu)
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (wa pili kushoto) akimpa maelezo Diwani wa Kata ya Majengo, Shufaa Ibrahim namna taka ngumu zinazosababisha uzibaji wa chemba za majitaka wakati wa ziara yake Machi 26, 2024 ya kutembelea kata hiyo na kujionea hali ya mazingira ilivyo. Kulia ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Bernard Rugayi.
MTUMISHI wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) Henry Motto, akinyonya majitaka yaliyotuama katika mtaa wa Kitenge kata ya Majengo jijini Dodoma Machi 26, 2024.
MKURUGENZI Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph (kulia) akiwa na Diwani wa Kata ya Majengo, Shufaa Ibrahim wakikagua miundombinu ya majitaka katika eneo hilo wakati wa ziara yake  Machi 26, 2024 ya kutembelea kata hiyo na kujionea hali ya mazingira ilivyo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira DUWASA, Mhandisi Bernard Rugayi. (Picha na Mpigapicha Wetu).

MAJALIWA ATAKA UWEKEZAJI ATCL UWE KICHOCHEO CHA UKUAJI WA UCHUMI


WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Uchukuzi kusimamia ipasavyo Shirika la Ndege Tanzania ili kuhakikisha uwekezaji mkubwa uliofanywa unaleta matokeo chanya na kuwa kichocheo cha ukuaji wa sekta nyingine mtambuka na uchumi kwa ujumla wake.
Amesema kuwa ongezeko la ndege na huduma za usafiri inasaidia kuongeza fursa za biashara kati ya Tanzania na mataifa mengine kuongeza upatikanaji wa fedha za kigeni na kuongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini.
Amesema hayo (Jumanne, Machi 26, 2024) alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 737-9 Max, kwenye uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Aidha Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa ili kuendelea kuikuza sekta ya anga nchini, Wizara ya Uchukuzi iandae mpango wa kuongeza wataalamu wazalendo katika fani zinazohusu masuala ya ndege hususan katika eneo la matengenezo na urubani.
Mheshimiwa Majaliwa amewataka watumishi wa Shirika la Ndege Tanzania kuongeza uzalendo na kuwafichua wale wote wenye nia ya kulihujumu shirika hilo pamoja na kudhibiti upotevu wa mapato kupitia tiketi na mizigo.

WAZIRI JAFO AFUNGUA BARAZA LA WAFANYAKAZI OFISI YA MAKAMU WA RAIS


WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewapongeza watendaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kufanya kazi kwa bidii na kudumisha Muungano.
Amewapongeza watendaji hao kwa kujituma katika kuwezesha kufanyika kwa vikao vya Masuala ya Muungano ambavyo vina kazi ya kujadili masuala ya Muungano.

Akifungua Mkutano wa Nne wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais Machi 26, 2024 jijini Dodoma, Dkt. Jafo amesema mafanikio ya utekelezaji wa majukumu hayo ni matunda ya ushirikiano baina ya watumishi katika Ofisi hiyo.
Amesema katika kuelekea miaka 60 ya Muungano yapo mengi ya kujivunia yakiwemo utatuzo wa chanamoto za Muungano kutokana na maelekezo ya viongozi wa kitaifa, ambayo kwa kiasi kikubwa ni matunda ya utendaji wa watumishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais

Pia, Waziri Jafo amewapongeza watendaji hao kwa kusimamia vyema miradi ya mazingira ambayo imewajengea wananchi uwezo wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

NAIBU WAZIRI MADINI ATETA NA NAIBU WAZIRI NISHATI WA MAREKANI


-Marekani yavutiwa kuwekeza Madini Mkakati Tanzania

-Naibu Waziri asema Tanzania mahali salama pa uwekezaji
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amekutana na kuzungumza na Ujumbe kutoka Marekani uliongozwa na Naibu Waziri wa Nishati wa Nchi hiyo Joshua Volz ambapo pia ameambatana na viongozi waandamizi kutoka Wizara ya Nishati ya Marekani pamoja na viongozi waandamizi wa Ofisi ya Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.

Kikao hicho, kimefanyika leo Machi 27, 2024 katika Ofisi Ndogo Wizara hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.

Akizunguza katika kikao hicho, Dkt. Kiruswa amesema Tanzania ni sehemu sahihi na salama ya Uwekezaji hususan katika Sekta ya Madini ambapo ameueleza ujumbe huo kuwa Serikali ya Tanzania iko tayari kulinda wawekezaji ili kuongeza tija katika maendeleo ya taifa.

Aidha, Dkt. Kiruswa amesema mpaka sasa nchi ya Tanzania imefanyiwa utafiti wa kina wa jiofizikia kwa kutumia ndege (high resolution airborne geophysical survey) kwa asilimia 16 pekee hivyo bado umuhimu na uhitaji mkubwa kufanyika tafiti zaidi Ili kuongeza wigo wa maeneo zaidi yatakayo pelekea kufunguliwa kwa miradi mipya ya uchimbaji madini.

Pamoja na mambo mengine, Dkt. Kiruswa amesema Serikali ya Tanzania kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) linawalea wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapa mafunzo na kuwasaidia kufanya tafiti ili kufanya shughuli zao kwa ufanisi.

Tuesday, March 26, 2024

WAKONGWE WA RTD WAZUNGUMZA NA WAZIRI NAPE


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Moses Nnauye (Mb.) amepongeza Umoja wa Watangazaji Wakongwe wa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) ambayo kwa sasa inatambulika kama TBC kwa kuanzisha umoja huo ambao utapeleka salamu kuwa ni kazi ya kistaarabu na ni sekta muhimu.

Mhe. Nape ameyazungumza hayo leo jijini Dar es Salaaam wakati wa kikao chake na Wakongwe wa Tasnia ya Habari nchini waliowahi kutangaza RTD wakati na baada ya Uhuru ambao kwa sasa ni wastaafu na wanachama wa Umoja huo.


“Redio Tanzania Dar es Salaam ni tunu ya Afrika kwa sababu ni chombo kilichoshiriki harakati za kupigania Uhuru wa Bara la Afrika, kuna historia nyingi ambazo hazijatamkwa hivyo ni muhimu zikazungumzwa kwa kuwa wahusika bado mpo”, amesema Waziri Nnauye.

Ameongeza kuwa Serikali ipo tayari kuwashika mkono ili Umoja huo uweze kutekeleza maono yao ya kuanzisha redio na Chuo cha Utangazaji na kuna wadau wa Wizara hiyo ambao wanaweza kuvutiwa na wazo hilo pia na kuamua kufadhili.

DKT. BITEKO ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MIKATABA UENDESHAJI MRADI WA EACOP



Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, Leo 27 Machi, 2024, ameshuhudia Utiaji saini mikataba mitatu ya utekelezaji wa mradi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP).

Mkataba wa Kwanza unahusisha ukodishaji wa eneo la kujenga Miundombinu ya kuhifadhi mafuta (Land Lease Agreement for Marine storage and Terminal Area) Kati ya TPDC na EACOP.
Mradi wa pili ni wa kutumia eneo la Maji (Marine user Rights) kati ya EACOP na Mamlaka ya Bandari Tanga na mkataba wa tatu ni wa kufanya shughuli za Bandari (Marine Facility Agreement) Kati ya TPA na EACOP.

Utiaji saini mkataba huo pia umeshuhudiwa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda Mhe Dkt. Ruth Nankabirwa.

WATUMISHI WA AFYA WATENGENEZEENI FIKRA NJEMA WANANCHI KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO : DKT. JINGU


Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt John Jingu amewataka watumishi wa afya kuwatengenezea fikra njema wananchi katika kukabiliana na magonjwa mbalimbali hasa magonjwa ya mlipuko ikiwemo ugonjwa wa Kipindupindu.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Machi 25, 2024 wakati akipokea taarifa ya sekta ya afya Mkoa wa Mwanza iliyowasilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Thomas Rutachunzibwa kuelezea hali ya huduma za afya katika mkoa huo.
Dkt. Jingu amesema ili kukabiliana na magonjwa ya mlipuko silaha kubwa ni kubadilisha fikra za wananchi kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kukabiliana na magonjwa hayo ikiwemo ugonjwa wa Kipindupindu ambao umekuwepo katika mkoa huo.

Aidha, Dkt Jingu amewataka watumishi hao kuzingatia ubora wa huduma za afya kwa wananchi kwa kuzingatia staha, utu na heshima na kuzitoa kwa ubora wake kwani serikali imeweka miundombinu rafiki kwa ajili ya kutolea huduma za afya nchini.